SHULE YA MSINGI CHEMKAYAPATIWA MSAADA

Shule ya Msingi ya Chemka iliyopo nje kidogo wa mji wa Bomang’ombe wilayani Hai imepokea majengo yaliyojengwa na Bibi Kizee wa Kijerumani Elisabeth Dorr(89) kupitia shirika la Ako lililoko mjini Moshi.


Shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Chemka ilipata ufadhili huo mwaka 2008 kupitia kanisa katoliki parokia ya Chekereni kupitia shirika la AKO-Moshi

Majengo hayo ni pamoja na madarasa matatu,nyumba mbili za walimu,bwalo la chakula,stoo na ofisi ya shule pamoja na kugharamia uunganishaji wa umeme na kuvuta maji ya bomba ambapo Bibi Dorr alitoa jumla ya Euro 50,000 ambazo ni sawa na shilingi 93,554,698.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo,David Mosha ameeleza kuwa Bibi huyo wa Kijerumani pia akatika fedha hizo alitoa madawati 66,meza 4,viti 4,makabati 7 ya ukutani,sufuria mbili kubwa,beata stoves 2,meza na mbenchi 15 kwa ajili ya matumizi ya bwalo

Mosha ameeleza kuwa awali Bibi huyo alijenga darasa moja mwaka 2008 na baadaye mwaka uliofuata alimtuma mwenyekiti wa Shirika la AKO-Tanzania,Klaus Boehme na kufurahishwa na usimamizi wa miradi hiyo shuleni hapo.

Akipokea rasmi miradi hiyo,Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga amewataka wakazi wa kijiji cha Chemka kuyatunza majengo hayo kwa nguvu zao zote na pia kuhakikisha wanaingia katika kampeni ya kupanda miti kutokana na eneo hilo kunyemelewa na jangwa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mifugo

Aidha Makunga amewataka kutumia fursa ya vyumba bora na vizuri pamoja na umeme kuchangia ununuzi wa kompyuta kwa ajili ya kuanzisha darasa la kompyuta pamoja na kurahisisha kazi za utawala.

Aliahidi kuchangia kompyuta moja kwa ajili ya kuanzia na kuongeza kuwa siyo kwamba kukiamilika kwa majengo hayo kutaifanya shule hiyo kufanana na shule za mjini lakini pia kutawaingia katika mazingira ya kisasa ya teknolojia zinazotumika katika maeneo ya mjini


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia