TANZANIA IPO CHINI KATIKA UZAJI WA NGOZI NJE YA NCHI
Imebainika kuwa pamoja kuwa Tanzanina ni nchi ya tatu kwa
kuwa na mifugo mingi duniani lakini ndio nchi ambayo ipo chini katika
kuzalisha la ngozi zenye ubora.
Hayo yamebainishwa jana na mkurugenzi wa taasisi ya
teknolgia ya ngozi ambayo makao makuu
yake yako jijini Dar es salaam Pro.John Kondoro wakati alipokuwa akifungua
mkutano wa siku sita wa wadau mbalimbali wanaozalisha ngozi hapa nchini pamoja
na wananchi wa Somalia
.
Alisema kuwa nchi yetu imekuwa ni nchi yenye mifugo mingi
lakini ndio nchi ambayo inaingizia nchi kipato kidogo kuliko sekta zote zile.
Alibainisha kuwa nchi yetu imekuwa ikizalisha ngozi nyingi
ambazo hazina ubora hali ambayo inafanya mpaka pato la ngozi ambalo linauzwa
nje ya nchi kuwa dogo kutokana na ngozi zetu kutokuwa na sifa ambazo
zinatakiwa.
“unajua unakuta ngozi
za wanyama wetu hazina ubora
kwani ngozi zingine mfugaji amepiga muhuri sehemu ambayo haikutakiwa
kupigwa muhuri ,wakati mungine ngozi zinakuwa na ukurutu ambao labda unakuta
ng’ombe yule au mfugo huyo aliugua na nyingine unakuta hajapewa chakula cha
kutosha hivyo pia hupelekea ngozi zetu kutokuwa na
ubora”alisema Pro.Kondoro
Kondoro alisema aliipongeza serekali yatu kwa kutengeneza
sera ya kuboresha ngozi ambapo alisema kuwa katika sera ya ngozi ya mwaka 2007 inazungumzia
maboresho ya ngozi ambapo wameweka asilimia ya ubora wa ngozi inayotakiwa
kuuzwa nje ya nchi ambapo awali ilikuwa
ngozi inayounzwa nje ya nchi inatakiwa kuwa asilimia 40%na kupandisha hadi
kufikia asilimia 90% kwa ngozi ambazo
zimechakatwa.
Kwa upande wake waandaaji wa semina hiyo Dr.Albert Mmari
alisema kuwa semina hii inalenga kuwapa uzoefu wa namna ya shughuli za
machinjio zinazofanywa ,namna ngozi zinavyoandaliwa na jinsi zinavyopimwa ubora
ambapo alibainisha kuwa watatembelea kituo cha machinjio cha jijini Arusha
(Arusha meet) kilichopo sakina.
Aliwataka wafugaji kutunza ngozi ikiwa ni pamoja na
kuangalia sehemu ambazo wanapiga mihuri mifugo yao
na kuwasisitiza wawapemifugo yao
chakula cha kutosha ili kuweza kuboresha ngozi hizo.
Adha alisema kuwa iwapo vyote hivyo vitafanywa basi pato la
taifa litaweza kuongezeka kupitia mifugo yetu ambapo aliongeza kuwa mkutano huu
umeshirikisha wadau kutoka mikoa mbalimbali hapa nchi wakiwemo kutoka mikoa ya
Kagera,Pwani,Mara,Musoma ,Arusha pamoja na wageni kutoka nchi ya Somalia.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia