WAKULIMA MILIONI MOJA WAPATIWA ELIMU YA KILIMO HIFADHI

Mkuu wa wilaya ya  Arumeru , Nyerembe Munasa akiwa anafungua mkutano wa wadau wa kilimo leo katika hotel ya Naura spring jijini hapa

SHIRIKA la mtandao wa kilimo hifadhi Afrika(ACT)limefanikiwa kuwafikia na kuwapatia wakulima zaidi ya Milioni Moja elimu ya kilimo hifadhi  huku kwa upande wa Tanzania wakulima zaidi ya Elfu thelahini nao wamepatiwa elimu ya kilimo hicho ili kuboresha zaidi Kilimo hicho.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika hilo Mhandisi Said Mkwomwa wakati alipokuwa akiongea na wakulima mbalimbali wa kanda za Afrika mashariki, Afrika ya kusini pamoja na Afrika ya kati.

Alisema kuwa wakulima hao wamepatiwa elimu hiyo ili kuweza kufanya kilimo ambacho kina tija zaidi tofauti na kilimo cha kawaida ambacho kimekuwa ni mzigo mkubwa sana kwa jamii.


‘ndani ya nchi hizi zipo baadhi ambazo zimeshafanikiwa sana lakini kwa upande wa Tanzania Kilimo hiki kipo ila hakijafanikiwa sana kutokana na wakulima wengi sana kutegemea kilimo cha asili ambacho kinahusisha zaidi mifugo,kitu ambacho kina haribu mazingira na wao wenyewe kuchoka sana sasa ni vema kama wakatumia zaidi hiki kilimo cha kuhifadhi mazingira ambacho kina faida sana kwa wakulima mbalimbali”alisema  Said

Alitaja faida kubwa sana ya kutumia aina kilimo hicho hapa nchini kuwa ni pamoja na kuhifadhi mazingira hasa maji yaliopo ardhini, huku pia aina hiyo ya kilimo ikisaidia kupunguza na kutatua changamoto mbalimbali za Mabadiliko ya Tabia za nchi ikiwemo ukame ambao umekuwa ni chanzo cha njaa kwa jamii.


Awali MKUU wa wilaya ya Arumeru , Nyerembe Munasa amewataka wakulima kuachana na kilimo cha mazoea badala yake kutumia  mfumo wa kilimo  hifadhi ambacho kimeonekana kuwa cha manufaa makubwa kwa wakulima wadogo barani Afrika na ulimwenguni kwani kimekuwa kikikabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .

Nyerembe alisisitiza kuwa, kilimo hicho kitawezesha kwa kiasi kikubwa sana kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao pamoja na kuondoa tatizo la njaa hususani katika maeneo ya vijijini kwani wakulima wengi hawana elimu hiyo kwani wengi wamekuwa wakitumia kilimo cha mazoea na kujikuta wakipata hasara kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamekuwa yakisababisha ukosefu wa mvua kwa maeneo mengi.

Aidha aliwashuri wakulima mbalimbali  Afrika kujenga mtandao wa kufahamiana  na kubadilishana uzoefu juu ya kilimo hicho na kuwataka wadau wa kilimo wajitokeza kusaidia maendeleo ya kilimo ili kukiwezesha kilimo hicho kuenea maeneo mengi hapa nchini

Pia alisema kuwa, kilimo hicho kinasaidia kuondoa wadudu waharibifu shambani ikiwa ni pamoja na  kuhifadhi mazingira na kumwezesha mkulima kuweza kulima kilimo chenye tija na kuongeza ubora katika kilimo hicho na hatimaye kuongeza hata mavuno

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia