UCHAGUZI UVCCM ARUSHA VURUGU TUPU CHATANDA ANUSURIKA KICHAPO
HALI ya tafrani imeibuka
katika uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm)
mkoa wa Arusha baada ya katibu wa CCM mkoani hapa,Mary Chatanda kunusurika
kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga uchaguzi huo kwa lengo la kumpitisha chaguo
lake ambaye alitajwa kuwa ni ,Dk Harold
Adamson.
Katika vurugu hizo Chatanda alinusurika kipigo kutoka kwa
wajumbe waliotoka wilayani ya Monduli baada ya kuamuru zoezi la uchaguzi huo
lilirudiwe kwa madai kwamba wajumbe hao pamoja na wale wanaotoka wilayani Meru idadi yao
ilikuwa na kasoro.
Katika
vurugu hizo makundi ya baadhi ya vigogo wa CCM hapa nchini
yanyohusihswa na waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu,Edward Lowasa pamoja
na Bernad Membe yalijidhihirisha waziwazi ambapo yalikuwa yakitambiana
nje ya ukumbi wa mkutano.
Hatahivyo,katika hali isiyo
ya kawaida polisi pamoja na maofisa wa usalama wa taifa waliwatimua waandishi
wa habari waliokuwa nje ya ukumbi wa mkutano katika jengo la CCM mkoani hapa
kwa amri ya katibu wa CCM wilaya kwa madai kwamba hawana mashati yenmye rangi
ya kijani.
Zoezi la kupiga kura za
uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa Uvccm mkoa lilianza majira ya saa 6;00
mchana ambapo upepo wa awali katika uchaguzi huo ulionyesha kwenda kwa
mgombea,Robinson Meitenyiku anayetokea wilayani Arusha.
Vurugu hizo zilianza majira
ya saa 9;00 mchana ambapo Chatanda alipoamuru wajumbe wa mkutano huo watoke nje
ya ukumbi kwa madai kwamba kuna baadhi yao
kutoka wilaya za Meru na Monduli walizidi.
Akitangaza uamuzi huo katibu
huyo alisema kwamba wajumbe kutoka wilayani Monduli idadi yao haikuwa halali pamoja na ile ya wilayani
Meru kwamba wajumbe watano walizidi kitendo kilichopingwa vikali.
Hatahivyo,mara baada ya
wajumbe hao kutoka nje ya ukumbi wa uchaguzi walianza kupaza sauti kwamba
katibu huyo analengo la kuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa anataka kumpitisha
mgombea wa nafasi hiyo,Dk Adamson.
Wakati vurugu hizo
zikiendelea ndipo baadhi ya wajumbe kutoka wilayani Monduli walitishia kumchapa
ndani ya ukumbi huo lakini juhudi zao zilizimwa na baadhi ya walinzi wakiwemo askari
wa jeshi la polisi mkoani Arusha.
Mmoja wa wajumbe hao kutoka wilayani
Monduli,Isaac Kadogoo alimwakia vikali Chatanda ndani ya ukumbi huo na
kumtuhumu kwamba kitendo chake cha kukaa karibu na sanduku la kura kilikuwa na
lengo la kutaka kuchakachua kura hizo.
“Mheshimiwa katibu rudi ukae
meza kuu hata kama wewe ni msimamizi wa uchaguzi huu ondoka hapo kwenye sanduku
la kura tuna wasiwasi na wewe”alisikika Kadogoo
Wakati hayo yakijiri nje ya
ukumbi wa mkutano huo baadhi ya wajumbe walipinga kitendo cha Chatanda kuwatoa
nje na kusema kwamba ana lengo la kuuvuruga uchaguzi huo ili chaguo lake
lipite.
Hatahivyo,ilipotimu majira ya
saa 9;15 mchana ndipo wajumbe hao walitangaziwa kurudi ndani ya ukumbi huo kwa
lengo la kurudia zoezi la kupiga kura na ndipo walipojipanga kwa mistari na
kuelekea katika ukumbi wa uchaguzi kupiga kura kwa mara nyingine.
Maofisa wa usalama wa taifa
sanjari na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha walikuwa wakiranda randa nje
na ndani ya ukumbi wa mkutano kuimarisha
ulinzi wakiwemo na baadhi ya maofisa wa Takukuru mkoani hapa.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia