MREMBO WA UTALII MANYARA KUPATIKANA OCTOBA 12

WANYANGE 14 wanatarajiwa kuchuana kwenye mashindano ya kumtafuta Miss Utalii wa Mkoa wa Manyara unaotaraji kufanyika Octoba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Kangaroo Hoteli Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.

Akizungumza jana na waandishi wa habari,Mratibu wa michuano hiyo Mosses Komba alisema maandalizi ya mpambano huo yameshakamilika na hivi sasa warembo hao wanafanya mazoezi kila siku kwa kupanda milima ya madini ya Tanzanite.

Komba alisema kupitia kampuni yake ya New Vision mashindano hayo yanatasindikizwa na mwanamuziki maarufu Wanne Star anayefanya muziki wake kwa kuimba na kucheza nyimbo za asili,Morgan Sound Band na Sarakasi.

Alisema michuano hiyo ya Miss Utalii mkoa wa Manyara inadhaminiwa na kampuni ya Ken Family General Trading Co,Radio 5,Kangaroo Hotel,Manga Gems,White Fashion,Manyara Inn na Baba G Intertainment.

Alisema warembo watakaoshikiri mashindano hayo ni wasichana wa wilaya zote tano za mkoa huo ikiwemo Simanjiro,Kiteto,Mbulu,Hanang’ na Babati ambao ni wanyange wa kiiraq,kimasai,kibarbaig na kifyomi.

Alitoa wito kwa watu wote wanaopendelea burudani za urembo kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo ili kuwaunga mkono wasichana hao wa mkoa wa Manyara ambao wote ni chipukizi katika masuala ya urembo.

“Lengo la mashindano hayo ni kuutangaza utalii wa ndani wa mkoa wa Manyara na ninawapongeza wazazi wa wasichana hawa wa mkoa wa Manyara kwa kuruhusu watoto wao wa kike kushiriki mashindano hayo,” alisema Komba.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia