WANAWAKE MKOA MANYARA WATAKIWA KUSHIRIKI ZAIDI KATIKA UCHIMBAJI WA MADINI

WANAWAKE wa Mkoa wa Manyara wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchimbaji wa madini kwa kujiunga kwenye vikundi vya ushirika ili waweze kujiinua kiuchumi kuliko kuwaachia wanaume peke yao.

Wito huo umetolewana Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Manyara Dorah Mushi wakati akizungumza na baadhi ya wanawake wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro waliompokea baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.

Mushi alisema wanawake wanaweza kujiinua kiuchumi kwa kujiunga kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya Dhahabu yaliyopo kata ya Daudi wilayani Mbulu au Tomarini ya kijani,gainet au Tanzanite yaliyopo wilayani Simanjiro.

Alisema wanawake hao wakijiunga kwenye vikundi vya ushirika wataweza kupatiwa mikopo itakayowawezesha kujishughulisha na uchimbaji wa madini ili waweze kuongeza kipato chao kuliko kuwaachia wanaume wachimbe peke yao.

“Mjitahidi kujiunga kwenye vikundi vya ushirika na mimi kama Mwenyekiti wa UWT wa mkoa nitawatafutia mikopo hivyo tutumie fursa hii kuunda ushirika ili mpate mikopo ya shirika la madini nchini Stamico,” alisema Mushi. 

Alisema umoja wao ndiyo nguvu yao na wasiwaachie wanaume peke yao kuhodhi fursa hiyo,hivyo kupitia vikundi vya ushirika watashirikiana kwa pamoja katika kujikomboa na hali ngumu ya uchumi inayowakabili.

Alisema wanawake wamekuwa wakinyanyasika kutokana na baadhi yao kuachiwa watoto na wanaume au baadhi ya wanaume kutojishughulisha hivyo kina mama kuwa na jukumu kubwa la kulea watoto wao peke yao.

Pia,Mwenyekiti huyo wa UWT aliwashukuru wanawake wa mkoa wa Manyara kwa kumchagua kila mara anapogombea nafasi yoyote kupitia mkoa huo hivyo atatumia fursa hiyo kwa kuwatumikia wanawake wote bila ubaguzi wowote.

“Watu walikuwa wanasema Manyara kuna ukabila mkubwa mimi siwezi kuchaguliwa na wabarbaig,wairaq,wafyomi na wamasai kwa vile mimi mchaga lakini hamkuangalia hilo nawashukuru sana mama zangu,” alisema Mushi.


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia