ARSENAL YAMUWEKA ZAHA KATIKA RADA ZAKE, KWA AJILI YA NAFASI YA THEO WALCOTT
Klabu
ya Arsenal iko katika mchakato wa kutafuta mchezaji atakayeziba pengo
la THEO WALCOTT baada ya kuingia katika kinyang’anyiro cha kutafuta
saini ya mchezaji wa Crystal Palace WILFRIED ZAHA. Aliyekuwa meneja
msaidizi wa Arsenal PAT RICE ambaye bado anafanya kazi na klabu hiyo
pamoja na kustaafu katika majira ya kiangazi alikuwa akimfuatilia
mchezaji mwenye umri wa miaka 19 katika mchezo ambao timu hiyo ilishinda
kwa mabao 4-3 dhidi ya Barnley Jumamosi. Arsenal katika kipindi cha
karibuni imekuwa ikituma wapelelezi wake katika michezo ya Palace
mahsusi kwa ajili ya kufuatilia kiwango cha Zaha hivyo kuwepo uwezekano
mkubwa wa kumyakuwa kinda huyo. ZAHA ambaye thamani yake inafikia kiasi
cha paundi milioni 12 anaweza kuwa mchezaji mpya kujiunga na Arsenal
kutokea katika ligi za chini kama klabu hiyo ikishindwa kumsainisha
WALCOTT mkataba mpya. WALCOTT ambaye mkataba wake umebakia miezi
isiyopungua 12 amekataa kusaini mkataba mpya ambao utakuwezesha kulipwa
kiasi cha paundi 75,000 kwa wiki ingawa bado wapo katika mazungumzo
zaidi kupata muafaka wa sakata hilo.
SUDAN YANYANG'ANYWA ALAMA NA FIFA.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia