Warembo
walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic.toka
kulia ni Magdalena Roy (Mshiriki namba 6,kutoka Dar City Center - Kanda
ya Ilala),Babylove Kalala (Mshiriki namba 9,kutoka Kagera - Kanda ya
Ziwa),Lightness Michael (Mshiriki namba 5,kutoka Dodoma - Kanda ya
Kati),Lucy Stephano (Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya
Kaskazini) na Diana Hussein (Mshiriki namba 20,kutoka Dar Indian Ocean -
Kanda ya Kinondoni.)
Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano ndie
alieweza kuibuka kinara wa Kinyang'anyiro cha Redd's Miss Photo Genic
2012.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa Mashindano ya
Miss Tanzanzia,Hashim Lundega akitangaza Mshindi wa Redd's Miss Photo
Genic ambaye ni Mshiriki kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy
Stephano (katikati).hafla ya shindano hilo ilifanyika jana usiku kwenye
Ukumbi wa hoteli ya E'Manyata Lodge,Monduli jijini Arusha.
Warembo walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo Genic
wakimshangilia mwenzao alieibuka mshindi wa Taji hilo mara baada ya
kutangazwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa
Mashindano ya Miss Tanzanzia,Hashim Lundega.
Warembo wenye vipaji vya kuimba wakitoa Burudani Mbele ya Warembo wenzao wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Photogenic 2012,Mroki Mroki asema
maneno machache kabla ya kuanza kutangaza tano bora ya Warembo
walioingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
Mkuu wa Itifaki na Nidhamu ya Miss Tanzania,Albert Makoye akitoa muongozo kwa warembo hao.
Mrembo
wa Mkoa wa Manyara, na mwakilishi wa Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano
usiku wa kuamkia leo amenyakua taji la Redds Miss Photogenic 2012 na
kuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la
Redds Miss Tanzania 2012.
Lucy amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2012.
Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki.
Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha Othman Michuzi na Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
Dalili za kuonesha kuwa Lucy amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa kwashangwe.
Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Magdalena Roy, Lightness Michael, Babylove Kalala, Diana Hussein na Lucy Stephano.
Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Oktoba 13 2012, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.
Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.
Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Stacy Mabula kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa.
Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Blue Peal Ubungo jijini Dar es Salaam Novemba 2, 2012.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia