DAKTARI ABAKA MGONJWA
ACCRA, Ghana
POLISI nchini Ghana wamemkamata dokta anayehusika na masuala ya
oparesheni za kusafisha vizazi (abortion), baada ya kutuhumiwa kumbaka
mwanamke aliyefika katika kituo chake kwa ajili ya kusafishwa ujauzito
wake.
Daktari huyo Joshua Dran anaaminika kubaka maelfu ya wanawake
kutokana na idadi kubwa ya wanawake ambao wamejitokeza hivi sasa wakidai
kufanyiwa vitendo hivyo na daktari huyo ambaye huwaomba kufanya ngono
ndipo afungue mifereji ya uzazi kwa ajili
ya kusafishwa.
ya kusafishwa.
"Kwa upande wake kulikuwa na bei maalum ya maelewano kwa ajili ya
utoaji mimba. Zaidi ada yake ilikuwa ni kati ya pesa ya Ghana yenye
thamani ya ¢50 na ¢100 ambayo aliichukua kabla ya oparesheni husika.
Kwa wateja wazuri kulikuwa na malipo ya ziada, daktari huyu alihitaji
ngono kabla ya kumsafisha mgonjwa, baadhi ya vyombo vya habari nchini
Ghana vimeripoti.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Dr Joshua Dran
amekanusha madai hayo, lakini alishangazwa na video ambayo iliwekwa na
wapelelezi wa kesi hiyo iliyomwonyesha yeye akimtendea mgonjwa wake
kitendo hicho kabla ya kumtoa mimba katika hospitali yake.
Dran anaendesha klinic ya Universal Mission Clinic iliyopo Madina
mjini Accra. Kiongozi mpelelezi katika kesi hiyo Anas Aremeyaw
Anas,aliwaambia waandishi wa habari kuwa "tulipokea kesi nyingi kutoka
kwa huyu bwana na alikuwa akitoa mimba za wanawake kinyume cha sheria za
nchi na suala hilo limepelekea vifo vya watoto wengi pamoja na matatizo
ya ugumba na hata wanawake wenyewe kufariki baadaye" alisema Anas.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia