MWANAMKE ACHOMWA MOTO KISA WIVU WA MAPENZI
MWANAUME mmoja nchini Nigeria anashikiliwa na polisi baada ya kummwagia petroli na kisha kumchoma moto aliyekuwa mkewe kutokana na wivu wa mapenzi.
Kehinde Adesamuye, 39, mkazi wa Lagos nchini Nigeria anadaiwa
kumchoma kwa moto wa petroli aliyekuwa mkewe Janet Udegba, 35 katika
mitaa ya Ikotun baada ya kuwa na hasira kutokana na kuhisi kuwa mkewe
huyo ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume
mwingine.
mwingine.
Janet alisema wakati wa tukio hilo alikuwa katika eneo lake la
biashara akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na
kumwagia petroli maeneo ya
mgongoni na kumwasha kwa kutumia njiti ya kibiriti.
mgongoni na kumwasha kwa kutumia njiti ya kibiriti.
Hata hivyo alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya kwake. Akisimulia mgogoro wao anasema;
"Mume wangu amekuwa na wivu daima. Amekuwa na tabia ya kunipiga kila
wakati pasipo kuomba msamaha. Nimejaribu mara nyingi kuachana
naye lakini yeye daima ananitisha kuwa lazima atanidhuru. Niliendelea
kuishi na yeye kwa kuwa nilikuwa na hofu na maisha yangu, aliwahi
kuniambia kuwa sitaweza kutoroka
hata siku moja.
hata siku moja.
"Mwezi uliopita nilimweleza kuwa nitaondoka na kwenda nje ya jiji la
Lagos, aliniruhusu na kudai kuwa hana tatizo na mimi ila aliniambia kuwa
atanifanyia jambo
moja ambalo sitakaa nikasahau, unaona alichonifanyia. Alitaka kuniua."
moja ambalo sitakaa nikasahau, unaona alichonifanyia. Alitaka kuniua."
"Nimekuwa nikifanya kazi ya kuuza vyakula katika eneo la kuzunguka
Ikotun. Kuna wanawake na wanaume pia wanaofanya biashara hii. Sisi wote
kwa pamoja ni kama marafiki wa kawaida tu.
"Mwishoni mwa wiki iliyopita mmoja kati ya wafanyabiashara wenzangu
alikuwa na sherehe ya mtoto wake, tulikwenda katika sherehe ile tukiwa
pamoja. Kehinde alikuwa huko pamoja nami, mmoja kati ya wafanyabiashara
wenzangu alinipa kinywaji, niliichukua kwa kuwa nilikuwa katika unywaji
pia."
Anasimulia Janet "hiyo ndiyo ulikumwa mwanzo wa tatizo, akasema kuwa
nilimbusu mtu mwingine mbele ya uwepo wake. Alisema kuwa nilikunywa
pombe ambayo mwanamume mwingine alikunywa. Tangu hapo alianza kunipa
onyo kwamba atakabiliana na mimi pindi tutakapofika nyumbani.
Janet anasema ili kuwa upande salama aliamua kumwita mdogo wake na
kumwambia kuwa aje kulala nyumbani mwake kwa usiku huo.Mimi sikutaka
kupigwa na mume wangu nilijaribu kumwelewesha lakini hakuelewa.
"Baada ya kufika nyumbani alianza kunilaani na kunitesa huku akiongea
kila aina ya neno mbele ya mdogo wangu. Lakini sikuweza kumjibu wala
kuongea lolote kwa kuwa sikutaka kugombana na yeye. Tabia hii iliendelea
hadi Jumamosi. Alinipiga hadi mateke kutoka kitandani lakini mimi
nililala juu ya sakafu.
"Nilipoamka siku ya Jumapili, alikuwa amekwenda nje. Niliingia bafuni
na kuoga haraka kwa kuwa sikuhitaji anikute akirudi. Lakini aliniwahi,
na kuanza kunipiga bila sababu ya msingi. Alinipiga sana mpaka
nikafikiria kuwa siku hiyo ataniua kabisa. Aliniacha baada ya baba
mwenye nyumba kuingilia kati ugomvi ule. Baada ya
kipigo kile niliondoka mpaka kwa mdogo wangu." alisema Janet.
kipigo kile niliondoka mpaka kwa mdogo wangu." alisema Janet.
"Serikali lazima ihakikishe kuwa Kehinde analipa kwa kile
alichonifanyia mimi. Mimi ni yatima. Sina mama, sina baba. Ninauza
biashara ya vyakula ili niishi. Sasa nimetumia pesa zangu zote kwa ajili
ya matibabu. Kwa kweli kwa sasa nahitaji msaada." alisema.
Akisimulia zaidi anasema baada ya kwenda kuishi kwa mdogo wake
aliendelea na shughuli zake, lakini Kehinde aliendelea kumfuata na
kumtaka amsamehe kutokana na kipigo alichompa.
Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili wamwombee msahama kwa Janet
lakini alikataa jambo lililopelekea Kehinde kumvizia akiwa katika
biashara zake na kumwagia petroli kisha kumchoma moto na kumsababishia
majeraha kadhaa nyuma ya mgongo wake mpaka
miguuni. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
miguuni. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia