MAINDI HUSABABISHA SARATANI YA INI

IMEBAINIKA kwamba Ugonjwa wa Saratani ya Ini inasababishwa na vijidudu ninavyo kula  Mahindi na Karanga Mashambani.
Vimelea vya vijidudu hivyo maarufu kama Aflatoxin ndiyo chanzo kikubwa cha ugonjwa wa Saratani ya Ini,unaosumbua Watanzania.
Ugonjwa wa Aflatoxin unaoshambulia mahindi na karanga, ambayo pia ndiyo chanzo kikubwa cha Saratani ya Ini
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa Kilimo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati unaonedelea hivi sasa katika Hoteli ya Ngurutodo jijini Arusha, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid alisema, kwamba Watanzania wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Ini kutokana na uchafu wa mazao na vyakula wanavyokula.
“Ugonjwa wa Saratani ya Ini inatokana na vimelea vya vijidudu vya Aflatoxin,vijidudu hivyo  vinapatikana  katika mahindi na karanga  na chanzo chake kikuu ni maeneo yenye uchevuchevu”alisema Naibu Waziri huyo na kuongeza:
“Ili watanzania waepukaane na ugonjwa huu, wanapswa  kuzingatia utunzaji wa vyakula vyao kuanzia mashambani hadi katika uandaaji wa unga wa ugali na uji”.
Akichangia mada katika Mkutano huo  Naibu Katibu Mkuu wa uzalishaji katika idara za kijamii Jesca Eriyo alisema kwamba, suala la utunzaji wa chakula inapaswa kuanzia katika ngazi ya familia.
“Kila mwanafamilia anapswa kutunza mazao katika hali ya usafi ili kuepukana na maradhi yanayosababishwa na vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya chakula ambayo pia ni hatari kwa afya za watumiaji”alisema Eriyo.


Katika hatua nyingine alisema kwamba, haina maana kutunza chakula ama mazao katika hali ya usafi wakati mifugo inaachwa ikizagaa ovyo kwani ukiepukana na uongjwa wa aflatoxin katika mazao utakutana nao katika mazao ya mifugo kama nyama,maziwa na mayai.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia