MAKANISA YACHOMWA MOTO MBAGALA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
VURUGU za waumini wa Dini ya Kislam na Wakristo zilizozuka leo katika eneo la Mbagala Majimatitu jijini Dar Es Salaam zimesababisha Makanisa matatu kuchomwa moto.
Vurugu hizo zilizotokana na utani wa watoto wadogo wenye umri wa miaka 12 zimesababisha waumini wa Dini ya Kislamu kuchoma makanisa hayo.
Utani wa watoto hao ulitokana na mtoto wa Kislamu kumwambia mtoto wa Kikristo kwamba kitabu chao wanachokiamini cha (Quran) kina nguvu kushinda kitabu cha Kikriston (Biblia) na kwamba ukikikojolea kitabu hicho unakuwa mwendawazimu (chizi,kicha).
Mashuhuda wa tukio hilo waliiambia tovuti hii ya Habarimpya kwamba baada ya watoto hao kubishana juu ya nguvu za Quran mtoto mwenye imani ya Dini ya Kikristo aliamua kukojolea kitabu hicho alichokuwa nacho mwenzake ili abaini kama kweli atakuwa chizi na baad ya hapo akamwambia mwenzake kuwa mbona hajawa chizi.Watu wakikimbia baada ya Askari Polisi kutawanya umati huo kwa mabomu ya machozi
Ramadhani Omaary Juma ambaye ni muuza matunda katika eneo hilo akizungumza na tovuti hii ya Habarimpya katika eneo hilo alisema kwamba, baada ya utani huo mtoto mwenye imani ya Dini ya Kislam alikimbia Msikitini na kuita wenzake kuwa kuna mtoto wa Kikristo amekojolea kitabu chao kitakatifu.
“Kwakweli haya yaliyotokea ni yakushangaza sana haiingii akilia kama utani wa watoto unaweza kuleta vurugu kiasi cha Makanisa kuchomwa moto na vita kubwa kuzuka katika eneo hilo na muda wowote mauaji yanaweza kutokea,haya yote yanatokana maamuzi ya ajabu watu hawa walipaswa kuuliza chanzo cha tukio hilo kwanza alisema Juma”.
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Salaam Suleimani Kova amesema kwamba Askari wa Jeshi la Polisi tayari wameweka kambi katika eneo hilo na kazi ya kutuliza vurugu hizo imeanza kufanikiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Meck Sadick alisema kwamba Serikali ikomakini katika suala hilo na kwamba hali ya utulivu itarudi katika maeneo hayo.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia